Imewekwa: 24th Oct, 2020
Bodi ya Maziwa Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) imewakutanisha kibiashara Ana kwa Ana (B2B meeting) wadau waliomo kwenye mnyororo wa thamani wa Maziwa kwa lengo la kujenga mahusiano mazuri ya kibiashara yatakayokuza na kuimarisha soko la maziwa nchini.
Mkutano huo wa siku moja ulifanyika katika Viwanja vya Maonyesho vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere vilivyopo jijini Dar es Salaam na ulihudhuriwa na wadau wapatao 90. Aidha wadau waliishauri Serikali kupitia Bodi ya maziwa kuongeza wataalamu wa Sekta ya Maziwa ili kukidhi mahitaji ya Wadau na kuziba ombwe la wataalamu wachache waliomo katika sekta.