Mshindi wa Kwanza Bodi za Serikali Maonesho ya Kilimo na Mifugo (Nanenane) 2024
Leading the Path
'Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa Kwa Maendeleo ya kIlimo na Mifugo'
NANENANE 2024
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (mwenye suti nyeusi) akipewa maelezo kuhusu mashine maalum ya kupandia mbegu za malisho ya Mifugo wakati wa Kilele cha Maadhimisho kitaifa ya Siku ya Unywaji maziwa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Furahisha mkoani Mwanza Juni 01, 2024.
WIKI YA MAZIWA MEI 28 - JUNI 01 2024
Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Prof. George Msalya akitoa neno la Utangulizi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda (hayupo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya 27 ya Wiki ya Unywaji Maziwa yaliyoanza Mei 28 hadi Juni Mosi 2024 ambapo amebainisha mchango wa sekta ya maziwa kwenye ajira kwakuwa zaidi ya kaya milioni mbili nchini zinajihusisha na uzalishaji na kuajiri watu kwani wadau zaidi ya elfu 7 wanajihusisha kwenye mnyororo wa thamani wa maziwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Bodi ya Maziwa Tanzania Prof. Zackaria Masanyiwa akitoa salamu mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda (hayupo pichani) wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya 27 ya Wiki ya Unywaji Maziwa yaliyofanyika leo Mei 29, 2024 katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, ambapo ametumia jukwaa hilo kuwaalika wafugaji kwenye viwanja hivyo ili kujifunza usindikaji na kuboresha mnyororo wa thamani wa maziwa