Bodi ya Maziwa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

TDB Logo
Dkt. Msalya : PUUZENI UPOTOSHAJI MAZIWA NI SALAMA
02 Oct, 2023
Dkt. Msalya : PUUZENI UPOTOSHAJI MAZIWA NI SALAMA

Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Dkt. George Msalya ameitaka Jamii ya kitanzania kuendelea kupuuzia watu wanaojitokeza kwenye mitandao na kupotosha kuhusiana na maziwa kusababisha magonjwa.

Ameyasema hayo Septemba 26, 2023 wakati wa Kongamano la wadau wa Maziwa jijini Mwanza liliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa ambapo amewasihi watanzania kuwasilikiliza Wataalamu wa sekta ya Maziwa na kuachana na wababaishaji wenye maslahi yao binafsi.

"Maziwa yanayozalishwa viwandani ni salama kwa matumizi ya binadamu, tuachane na hawa wababaishaji wanaojitokeza kupotosha Jamii, nchi yetu imetupa uhuru wa kusema lakini uhuru huu tuutimie kusema mambo yenye tija" Amesisitiza Dkt. Msalya

Amesema kuwa Maziwa ni chakula chepesi hasa kwa watoto hivyo ametoa wito kwa wazazi kutilia mkazo lishe ya watoto kwa ajili ya ukuaji mzuri wa mtoto kwani anapokuwa na afya bora humpelekea hata kufanya vizuri kitaaluma.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Bodi ya Maziwa Prof. Zacharia Masanyiwa amesisita kuwekeza katika afya ya mtoto kwa maendeleo ya baadaye hasa katika miaka mitatu ya mwanzo ya ukuaji wake kwakuhakikisha lishe yake inaambatana na maziwa.

Kongamano la Wadau wa maziwa ndio jukwaa pekee linaloweza kuwakitanisha wadau mbalimbali na  walioko kwenye mnyororo wa thamani wa maziwa kujadili maendeleo ya Tasnia ya Maziwa hapa nchini.