Bodi ya Maziwa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

TDB Logo
KAMPENI YA UNYWAJI MAZIWA YAFIKIA WANAFUNZI ZAIDI YA LAKI MOJA NCHINI
18 Nov, 2024
KAMPENI YA UNYWAJI MAZIWA YAFIKIA WANAFUNZI ZAIDI YA LAKI MOJA NCHINI

Kampeni ya Mpango wa Unywaji Maziwa Shuleni inayotekelezwa na Bodi ya Maziwa Tanzania Kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali hapa nchini imewafikia zaidi ya wanafunzi laki moja walioko katika Shule 140 za Msingi na Sekondari hapa nchini.

Hayo yameelezwa Novemba 14, 2024 na Kaimu Meneja Masoko wa Bodi ya Maziwa Bw. Joseph Semu alipokuwa akitoa tathimini ya Mpango wa Unywaji Maziwa Shuleni akiwa jijini Mbeya ambapo Bodi ya Maziwa Tanzania imepita kufanya ukaguzi na tathimini ya Utekelezaji wa  Mpango huo unaotekelezwa Kwa kushirikiana na Wasindikaji waliopo Mkoani Mbeya kwa baadhi ya Shule zilizopo Mkoani humo.

"Serikali imekuja na kampeni hii lengo likiwa kuhakikisha inalinda Afya za wanafunzi na kupunguza tatizo la udumavu na utapiamlo Shuleni" Amesema

Semu amesema mbali na kuwafikia wanafunzi hao zaidi ya laki moja lakini serikali  inaendelea na jitihada za kuwafikia wanafunzi wengi zaidi hapa nchini kwani Kwa sasa ni Shule 140 tu ndio zinazotekeleza Mpango huo nchi nzima.

Mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya Msingi Mwenge Reuben Fredy amesema ili serikali iweze kufikia malengo iongeze bajeti Shuleni ili wanafunzi wote wapatiwe Maziwa bure.

Naye Daktari wa Mifugo Mkoa wa Mbeya, Samora Mshang'a amesema kupitia kampeni hiyo Mkoa wa Mbeya utashirikiana na Bodi ya Maziwa Tanzania kuhakikisha wanafikia malengo ya Uhamasishaji matumizi ya Maziwa Shuleni.