Bodi ya Maziwa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

TDB Logo
MAADHIMISHO 26 YA WIKI YA MAZIWA KITAIFA KUFANYIKA TABORA
26 May, 2023
MAADHIMISHO 26 YA WIKI YA MAZIWA KITAIFA KUFANYIKA TABORA

Kuelekea katika kuadhimisha ya Wiki ya Maziwa Kitaifa mkoani Tabora, Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe.Balozi Dkt. Batilda Salha Burian ametoa wito kwa wadau wote wa tasnia ya Maziwa na wananchi wote kwa ujumla kutumia fursa mbalimbali kwenye maadhimisho hayo. Kwani maadhimisho haya yatakuwa na malengo ya kukuza ufanisi katika uzalishaji wa Maziwa yenye ubora.
 
Kwa Mwaka huu wa 2023, Wiki ya Maziwa kitaifa yenye kauli mbiu “Maziwa salama, Afya yetu” yatafanyika mkoani Tabora, Manispaa ya Tabora kuanzia tarehe 29/05/2023 hadi tarehe 01/06/2023, yatafunguliwa na Mhe. David Ernest Silinde (MB), Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Siku ya Kilele yatafungwa na Mhe. Abdallah Hamis Ulega (MB), Waziri wa Mifugo na Uvuvi.