Prof. Msalya: WAANDISHI WA HABARI TUMIENI KALAMU ZENU KUELIMISHA JAMII UMUHIMU WA UNYWAJI MAZIWA
Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Profesa Msalya amewataka Waandishi wa vyombo vya Habari hapa nchini kitumia kalamu zao katika kutoa elimu Kwa jamii kuhusu umuhimu wa unywaji maziwa na namna yakuyatunza kabla ya kumfikia mlaji.
Prof Msalya ameyasema hayo Mei 21, 2024 wakati akitoka mada katika warsha ya Waandishi wa Habari iliyofanyika katika ukumbi wa TVLA jikoni Dar es Salaam yenyewe lengo la kuwajengea uwelewa wanahabari kuhusu Tasnia ya Maziwa kuelekea Maadhimisho ya 27 ya Wiki ya Maziwa yanayotarajiwa kufanyika mkoani Mwanza
"Waandishi wa Habari ni kalamu zetu ambazo tunazipeleka Kwa jamii Kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu umuhimu wa Maziwa na namna Bora ya kuyatunza kabla ya kumfikia mlaji" Amesema Prof. Msalya
Prof. Msalya amesema kuwa Maziwa Bora yaliyopo nchini ni asilimia 12 ambayo yanaingia kwenye mfumo rasmi Kwa kuyapeleka katika vituo vya kukusanyia Maziwa vilivyopo 252 nchini.
Ameeleza kuwa ili kuhakikisha wanafikia malengo serikali kupitia Benki ya Kilimo Tanzania (TADB) wamekuwa nautaratibu wa kukopesha watu, Taasisi Kwa ajili ya kuvisaidia viwanda kuimarika pamoja na mifumo ya kukusanyia Maziwa.
Profesa Msalya ameishukuru serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya ufugaji wa ng'ombe wa Maziwa na kufanya uwekezaji katika mnyororo wa thamani wa Maziwa.
Kila mwaka tangu 1998 WMU, TDB na wadau wake wanafanya Maadhimisho ya unywaji maziwa Kwa kuonesha shughuli za uwekezaji na ujasiriamali katika Tasnia ili kuwavutia watu wengi wapende shughuli za Tasnia lakini zaidi kupenda kutumia Maziwa na bidhaa zake.
Kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya Habari katika kuhabarisha umma TDB Kwa kushirikiana na wadau wake imeandaa semina hiyo ili kujenga uwelewa wa pamoja kuelekea Maadhimisho ya 27 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza kuanzia Mei 28, 2024 mpaka Juni 01, 2024.