Bodi ya Maziwa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

TDB Logo
TADB YAVIMWAGIA MABILIONI VIKUNDI VYA UZALISHAJI MAZIWA NCHINI
02 Oct, 2023
TADB YAVIMWAGIA MABILIONI VIKUNDI VYA UZALISHAJI MAZIWA NCHINI

Serikali kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya Tsh. 1.02 Bil. kwa wafugaji wadogo na vikundi vya Uzalishaji Maziwa nchini Kwa ajili ya ununuzj wa ng'ombe bora wa maziwa.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa TADB Bw. Marick Edmund alipokuwa akitoa salamu za Benki hiyo kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Unywaji Maziwa Shuleni yaliyofanyika kitaifa Jijini Mwanza katika Viwanja vya Furahisha Septemba 27, 2023, ambapo lengo la kutoa fedha hizo nikuwawezesha wafugaji wadogo na vikundi vya Uzalishaji Maziwa kununua ng'ombe bora wa maziwa wapatao 398 watakaopelekea kuongeza uzalishaji wa maziwa hapa nchini.

"Kupitia 9 AMCOs na vikundi vya Uzalishaji Maziwa (5 AMCOs toka Tanga, 2 Kilimanjaro, 1 Arusha na Mbeya) serikali imewekeza fedha zake hapo ikiamini kuwa kupitia vikundi hivi itasaidia kuongeza hali ya upatikanaji wa maziwa hapa nchini" Ameongezea Bw. Edmund.

Pia TADB kupitia mradi wake wa TI3P imeweza kutoa ruzuku ya asimilia 25 ya gharama za Mitamba yenye thamani ya Tsh. 257,256,625 ili kumpunguzia mzigo wa gharama ya mkopo na uendeshaji mfugaji mdogo wa ng'ombe wa maziwa ili aweze kumuhudumia na kuongeza uzalishaji na tija.

Katika hatua nyingine, TADB imekabidhi mfano wa hundi ya Tsh. 257,256,825 kwa mwenyekiti wa wa UWAKO AMCOs cha Korogwe mkoani Tanga ambaye ni mmoja wa wanufaika wa Mkopo wa ununuzi wa ng'ombe wa maziwa na ruzuku iliyotolewa na benki hiyo.