Bodi ya Maziwa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

TDB Logo
TDB YATEMBELEA SHAMBA LA NG'OMBE WAMAZIWA( MIDLAND ESTATE DAIRY FARM) WILAYANI BAHI, MKOA WA DODOMA
11 Jan, 2024
TDB YATEMBELEA SHAMBA LA NG'OMBE WAMAZIWA( MIDLAND ESTATE DAIRY FARM) WILAYANI BAHI, MKOA WA DODOMA

Yatoa Elimu ya Kitaalamu juu ya Ufugaji wa Kibiashara na elimu ya Soko la Maziwa nchini

 

Timu ya Wataalamu toka Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) Januari 10, 2024 imetembelea shamba la ng'ombe wa maziwa la Midland lililopo wilayani Bahi, mkoa wa Dodoma na kutoa elimu ya kitaalamu juu ya ufugaji wa ng'ombe wa maziwa kibiashara na elimu ya namna yakutafuta soko la Maziwa hapa nchini.

Akitoa elimu hiyo,  Mtekinolojia wa Chakula Bi. Neema Moshi amemtaka mmiliki wa shamba hilo Bw. Merius Kabunga kutumia wataalamu wa mifugo mara kwa mara katika kutibu na kutoa huduma kwa mifugo shambani kwani kwakufanya hivyo kutamuwezesha kuweka kumbukumbu sahihi za magonjwa, matibabu, uzalishaji, masoko na uzazi katika shamba hii itasaidia kuboresha hali ya afya ya Mifugo.

Pia ameshauri juu ya kufanya chanjo za magonjwa mara utokeapo mlipuko wa magonjwa ya mifugo hata kama ugonjwa huo haujasambaa katika eneo lake hii itasaidia kuikinga mifugo na magonjwa hayo ya mlipuko.

Naye Mkurugenzi wa shamba hilo Bw. Merius Kabunga ameishukuru sana Bodi ya Maziwa Tanzania kwakutembelea shamba lake nakumpa utaalamu wa namna yakukabiliana na magonjwa yatokanayo na ng'ombe wa maziwa na kuahidi kuwa ataendelea kushirikiana na TDB ilikupata uzoefu zaidi ikizingatia yeye ni mgeni kwenye Tasnia hii ya Maziwa.

Vilevile ameiambia Bodi kuwa hivi karibuni amejipanga kufungua vituo viwili vya kuuzia maziwa hapa Dodoma ili kuunga juhudi zinazofanywa na Bodi ya Maziwa Tanzania katika kuhamasisha Unywaji wa Maziwa yaliyo safi na  salama kwa afya ya watanzania.

Bodi ya Maziwa Tanzania ni chombo Cha serikali kilichopewa dhamana yakusimamia sekta ya Maziwa hapa nchini ambapo Kwa mwaka huu imejipanga kutoa mafunzo juu ya  elimu ya ufugaji bora, kuandaa na kuhifadhi malisho pamoja na utambuzi wa magonjwa pamoja na kusaidia upatikanaji wa soko la Maziwa hapa nchini.