Bodi ya Maziwa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

TDB Logo
TDB YATOA RAI KWA WANANCHI WA MTWARA KUTUMIA FURSA YA UFUGAJI WA NG'OMBE WA MAZIWA
01 Oct, 2024
TDB YATOA RAI KWA WANANCHI WA MTWARA KUTUMIA FURSA YA UFUGAJI WA NG'OMBE WA MAZIWA

Bodi ya Maziwa Tanzania imewataka wananchi wa Mkoa wa Mtwara kutumia fursa ya ufugaji wa ng'ombe wa Maziwa ili waweze kujiongezea kipato kwakuwa uhitaji wa Maziwa kwa Mkoa wa Mtwara ni mkubwa ukilinganisha na mikoa mingine hapa nchini.

Rai hiyo imetolewa na Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Prof George Msalya wakati akitoa salamu za TDB kwenye kilele Cha Maadhimisho ya Siku ya Unywaji Maziwa Shuleni iliyofanyika Septemba 25, 2024 ambapo Mkoa wa Mtwara ulikuwa mwenyeji wa Maadhimisho hayo.

"Hapa Mtwara Kuna fursa ya ufugaji wa ng'ombe wa Maziwa ambapo Kwa mwezi unaweza kujipatia kipato Cha wastani wa Milioni moja mpaka mbili ambayo ni zaidi ya mshahara wa watu wengine" Amesema Prof Msalya

Ameeleza kuwa Uzalishaji mdogo wa Maziwa nchini umetajwa kuwa sababu kubwa ya kutofikia malengo  kwakuwa Tanzania Kwa sasa inazalisha Maziwa Lita bilioni 3.9 ambayo ni kidogo na hayatoshi kwa Kila mtanzania kunywa Lita 200 Kwa mwaka ambazo zimependekezwa na mashirika ya Afya na chakula duniani ya WHO na FAO.

Naye Ruth Mkopi, Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ametoa wito Kwa viongozi wa Mkoa kuhamasisha ufugaji katika Mkoa wa Mtwara kwani Kuna uhitaji wa kuimarisha Afya za watoto na jamii mzima kwa kupata Maziwa

"Niwaombe kupata fursa za uwezeshwaji wa kupata ng'ombe Bora ambao wanaweza kutoa Maziwa mengi ili kuendelea kuhamasisha Unywaji wa Maziwa na Uzalishaji wa Maziwa" Amesema Bi. Mkopi

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Abdallah Mwaipaya, akisoma hotuba Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ameiomba Bodi ya Maziwa Tanzania kuona namna ya kuweka bei rafiki ya Maziwa Kwa ajili ya wanafunzi ili Kila mwanafunzi aweze kumudu bei na kunywa Maziwa Kwa ajili ya kuupa mwili Afya, akili na nguvu ikizingatiwa wanafunzi wengi huenda Shuleni bila kupata chakula Asubuhi.

Ikumbukwe yakuwa Siku ya Unywaji Maziwa Shuleni huadhimishwa Kila Jumatano ya mwisho wa mwezi Septemba ambapo inasadikiwa kuwa siku hiyo wanafunzi wote duniani wanakuwa wapo Shuleni, Kwa mwaka huu 2024 yamefanyika Kitaifa Mkoani Mtwara na kubeba kauli mbiu "Mpe Mtoto Maziwa Kwa Maendeleo Bora Shuleni"