Imewekwa: 24th Oct, 2020
Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) inawaalika wadau wote wa Sekta ya Maziwa na Jamii kwa ujumla kutembelea banda letu kwenye Maonyesho ya 42 ya Kibiashara ya kimataifa ( Sabasaba) yaliyoandaliwa na TANTRADE yatakayofanyika katika Viwanja vya Sabasaba kwanzia tarehe 28/06/2018 hadi tarehe 8/07/2018. Bodi ya Maziwa itakuwa kwenye Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Jengo la IPP nyuma ya Jengo la NSSF.
TDB inalojukumu la kuhamasisha, kusimamia na kuratibu maendeleo ya tasnia ya maziwa nchini. Hivyo katika maonesho itajielekeza kwenye kutoa elimu, kuunganisha wadau (mikutano ya Biashara B2B), kusajili wadau, kutakuwa na siku maalumu ya maziwa na kutoa ufafanuzi wa changamoto za wadau. Pia utatolewa ushauri wa kitaalamu katika ufugaji wa ngo’mbe wa maziwa, usindikaji wa maziwa, biashara ya maziwa, n.k .
Wote Mnakaribishwa
Kunywa Maziwa, Furahia Maisha