Bodi ya Maziwa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

TDB Logo
DKT. KIJAJI AWATAKA WAFUGAJI NCHINI KUONDOKANA NA UFUGAJI HOLELA
02 Jun, 2025
DKT. KIJAJI AWATAKA WAFUGAJI NCHINI KUONDOKANA NA UFUGAJI HOLELA

Waziri wa mifugo na uvuvi Dkt.Ashatu Kijaji amewataka wafugaji nchini kuondokana na ufugaji holela ilikuondokana na migogoro isiyoyalazima

Waziri Kijaji amesema hayo wakati akifunga maadhimisho ya 28 ya wiki ya maziwa iliyofanyika Kitaifa Mkoani Morogoro ambae amebanisha kuwa Serikali imepunguza changamoto ya upatikanaji wa ng’ombe bora wa maziwa kwa kuwezesha kuzalisha jumla ya mitamba bora 3482 ya maziwa katika mashamba matano ya Serikali na mashamba nane ya sekta Binafsi 2024/2025.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima amesema mikakati iliyopo kati ya Mkoa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ni kuhakikisha mkoa wa Morogoro unakuwa kinara wa uzalishaji wa Ng’ombe bora na unywaji wa maziwa.

Nae Msajili wa Bodi ya Maziwa Prof George Msalya amesema kuwa kwasasa kuna ATM 16 za maziwa nchini na wataendelea kuongeza hamasa ya uzalishaji na unywaji wa maziwa ambapo wanakusudia kuweka ATM ya Maziwa Mkoani Morogoro