Dkt. MHINA AWATAKA WATUMISHI KUZINGATIA WELEDI, UAMINIFU NA WAJIBU.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Mhina amewataka watumishi wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) kuzingatia weledi, uaminifu na wajibu katika kutekeleza majukumu yao.
Ameyasema hayo Aprili 15, 2025 wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha menejimenti pamoja na watumishi wa bodi hiyo kilichofanyika katika moja ya ukumbi ziliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Dodoma.
Aidha, Dkt Mhina ameipongeza TDB kwa kuendelea kupiga hatua katika utoaji huduma zilizo bora na amewasisitiza kuwa ili kupata maendeleo ni wajibu wa kila mtumishi kufanya kazi kwa bidii.
Kwa upande wake Msajili Mkuu wa TDB Prof. George Msalya amesema kuwa Tasnia ya Maziwa inazidi kukua nchini na mpaka sasa kuna zaidi ya viwanda 152 vya uchakataji maziwa.
Vile vile ameongeza kuwa ipo mipango mbalimbali inayoandaliwa na kuratibiwa na bodi hiyo itakayolenga kuhamasisha unywaji maziwa nchini pamoja na manufaa yake.