MAFUNZO KWA VITENDO YAVUTIA WANANCHI BANDA LA BODI YA MAZIWA SABASABA

Wananchi kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam wameonesha kuvitiwa na mafunzo yanayotolewa na Wataalamu wa Bodi ya Maziwa Tanzania kuhusu kuhakiki ubora wa Maziwa wakati wa Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Kibiashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 5, 2025.
Mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uelewa wananchi wanaokuja kutembelea Banda la TDB yanawasaidia kuweza kutambua Maziwa yaliyoanza kuharibika na kuwekewa vitu vya ziada ambavyo ni hatari kwa afya ya mtumiaji.
Mtekinolojia wa Chakula kutoka Bodi ya Maziwa Tanzania Bw. Anthony Msaki amewataka wananchi kuwa makini na maziwa yanayouzwa kiholela huko mtaani ambayo hayajahakikiwa ubora wake hivyo amewasihi kuwa na vifaa vyakupimia ubora wa maziwa majumbani kwao kwani upatikanaji wake ni rahisi na anawezakuvitumia mtu yoyote.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi waliotembelea Banda la TDB wameshukuru kwa elimu walioipata ya namna ya kupima ubora wa maziwa kwani hawakuwa wanajua hatari za kiafya zakutumia maziwa yanauzwa mtaani kwenye chupa za maji.
Bodi ya Maziwa ipo katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara maarufu kama Sabasaba ambapo kwa mwaka huu imebeba Kauli mbiu isemayo Maonesho ya Kibiashara yakimataifa Sabasaba Fahari ya Tanzania