Bodi ya Maziwa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

TDB Logo
MDAU WA TASNIA YA MAZIWA NCHINI ASHINDA TUZO YA UBUNIFU NA UTOAJI AJIRA KWA VIJANA NA WANAWAKE 
25 Nov, 2024
MDAU WA TASNIA YA MAZIWA NCHINI ASHINDA TUZO YA UBUNIFU NA UTOAJI AJIRA KWA VIJANA NA WANAWAKE 

Mdau wa Tasnia ya Maziwa nchini Tanzania na Msindikaji wa kiwanda cha maziwa ya Sebadom mkoani Mbeya Bi. Anath Kombeson ameshinda tuzo ya ubunifu na utoaji ajira kwa vijana na wanawake inayotolewa na Graca Machel Trust chini ya program yake ya kuwainua Wanawake kiuchumi iliyo chini ya mke wa aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Bi.Graca Machel. 

Tuzo hiyo imetolewa hivi karibuni Johannesburg nchini Afrika Kusini  ikiwa na lengo la kuwainua kiuchumi Wanawake Wajasiriamali wa Kiafrika kwa kuwawezesha kukuza biashara zao na jamii kwa ujumla. 

Katika tuzo hizo zilizoshindanisha wanawake wajasiriamali kutoka nchi Saba za Kiafrika Tanzania ikiwa moja wapo, Bi. Anath ameshinda katika kipengele cha Utengenezaji wa Ajira Mpya 2024. 

Halfa hiyo ilihudhuriwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bi. Sauda Msemo.