Bodi ya Maziwa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

TDB Logo
TDB YADHAMIRIA KURASIMISHA TASNIA YA MAZIWA KWA VITENDO
17 Jun, 2025
TDB YADHAMIRIA KURASIMISHA TASNIA YA MAZIWA KWA VITENDO

Bodi ya Maziwa Tanzania imedhamiria kurasimisha Tasnia ya Maziwa kwa vitendo kwa kugawa vifaa vya kubebea maziwa (Milk Kens) kwa vikundi vitatu vinavyojihusisha ya usindikaji wa maziwa hapa nchini wakati wa Maadhimisho ya 28 ya Wiki ya Maziwa yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kiwanja cha Ndege mjini Morogoro.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa wasindikaji hao, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amewataka wanufaika wa vifaa hivyo kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ilikulinda ubora wa maziwa na kulinda afya ya mlaji.

"Maziwa yetu yanapoteza ubora Kwa sababu yanawekwa kwenye vyombo ambavyo havitakiwi kisheria, ninyi mmepewa vifaa hivi ilimtusaidie kuwaonesha wafanyabiashara wengine wa maziwa kuwa wanatakiwa kutumia vifaa bora vyakuhifadhia Maziwa Kama hivi, hivyo tunaamini mtakuwa mabalozi wema huko kwenye maeneo yenu" amesema Waziri Kijaji

Pia Mheshimiwa Waziri ametumua fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara wote wanaojihusisha na biashara ya Maziwa kutumia vifaa bora vinavyopatikana hapa nchini hii itasaidia kurasimisha sekta ya Maziwa kwa haraka.

Bi. Theresia Jacob kutoka kampuni ya Balima Food Product kutoka mkoani Morogoro ni mmoja wa wasindikaji wadogo waliopokea vifaa hivyo ameishukuru TDB Kwa namna inavyowasaidia na kuwainua wasindikaji wadogo kwakuwapa elimu ya kitaalamu ya namna bora ya usindikaji maziwa na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao.

Vilevile Mheshimiwa Waziri alikabidhi vyeti vya usajili kwa Bw. Aminael Maro Mzalishaji wa Maziwa na Bi. Jasmine Mrisho ambaye ni Mfanyabiashara wa Maziwa wote wakiwa ni wakazi wa  Mkoa wa Morogoro 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akikabidhi Cheti cha Usajili kwa Mzalishaji wa Maziwa Bw. Aminiel Maro wakati akifunga Maadhimisho ya 28 ya Wiki ya Maziwa yaliyofanyika Kitaifa mkoani Morogoro

Picha ya pamoja ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt Ashatu Kijaji pamoja na Viongozi wengine mara baada ya kukabidhi kifaa maalumu cha kubebea maziwa kwa Meneja Masoko wa Mama O Dairies Bw. Kephas Gembe wakati wa Maadhimisho ya 28 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa yaliyofanyika Mkoani Morogoro Juni Mosi 2025