Bodi ya Maziwa Tanzania
Wizara ya Mifugo na Uvuvi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

TDB Logo
TDB YALETA TABASAMU KWA WATOTO WENYE UHITAJI MAALUMU GEITA
25 Sep, 2025
TDB YALETA TABASAMU KWA WATOTO WENYE UHITAJI MAALUMU GEITA

Bodi ya Maziwa Tanzania kupitia Maadhimisho yake ya  Siku ya Unywaji Maziwa Shuleni imeleta tabasamu Kwa watoto wenye uhitaji maalumu mkoani Geita Kwa kuhamasisha Unywaji  wa Maziwa kwa wanafunzi walioko kwenye shule na vituo vyenye watoto wenye uhitaji maalumu.

‎Tukio hilo lililofanyika Septemba 22, 2025 mkoani Geita limehusisha watoto zaidi ya 300 walioko kwenye shule na vituo vinavyolea watoto yatima ambapo TDB Kwa kushirikiana na wadau wake wa Maziwa nchini wameweza kuwafikia watoto hao na kuwapatia elimu juu ya umuhimu wa Maziwa katika ukuaji wao.

‎‎Akizingumza Kwa niaba ya Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania , Bi. Dorinidei Mng'ong'o ambaye ni Kaimu Meneja Ufundi Maziwa amesema kuwa mtoto anapopata angalau glasi moja ya Maziwa Kwa siku inamfanya kupata virutubisho vinavyohitajika katika kujenga mwili na kumfanya kuwa imara.

‎‎Vilevile amesema kuwa pamoja na kupata virutubisho vya mwili lakini huwafanya watoto kuwa wenye furaha muda wote kwakuamini kuwa Kuna watu nyuma Yao wanaowapenda na kujali ilikutimiza ndoto zao.

‎‎Wakizungumza Kwa nyakati tofauti walezi wa vituo hivyo wameishukuru Bodi ya Maziwa Tanzania kwakuwakumbuka watoto hao na kuona umuhimu wa kuwatembelea na kuwapa elimu ya umuhimu wa Maziwa sambasamba na kuwapa Maziwa ili waendelee na utamadumi wakutumia Maziwa wangali bado wadogo.

‎‎Bodi ya Maziwa Tanzania kila Jumatano ya mwisho wa mwezi wa Septemba ya Kila mwaka huungana na mataifa mbalimbali ulimwenguni kuadhimisha siku ya Unywaji Maziwa Shuleni kwakuhamasisha jamii hasa watoto washule juu ya matumizi ya Maziwa na bidhaa zake ambapo Kwa mwaka 2025 siku hii inatarajiwa kufanyika Septemba 24 Mkoani Geita.