TDB YANGA'AA BODI YA MAZAO YA MIFUGO NANENANE KITAIFA 2025

Bodi ya Maziwa Tanzania imeongoza na kupata tuzo ya Mshindi wa kwanza katika kundi la Bodi za Mazao ya Mifugo wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma
Tuzo hiyo iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Agosti 8, 2025 wakati akihitimisha Maonesho ya Kimataifa ya Nanenane kwa mwaka 2025 itaongeza hari ya mabadiliko katika Tasnia ya Maziwa nchini.
Akiongea baada ya kupata tuzo hiyo Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Prof George Msalya ametoa Rai wa Wadau wa Maziwa nchini kuendelea kufuata Sheria na Kanuni zinazotakiwa ili Tasnia ya Maziwa nchini iendelee Kuchangia katika pato la Taifa.
Pia ametumia Fursa hiyo kuwapongeza Watumishi wote Kwa ushirikiano wakati wote wa maandalizi wa Maonesho haya kwani ubunifu na juhudi walizozionesha wakati wa kutoa elimu na huduma kwa wananchi waliokuwa wanatembelea banda la TDB zimepelekea kupata tuzo hiyo
Mtekinolojia wa Chakula kutoka Bodi ya Maziwa Tanzania Bw. Rajilan Hilal kwa niaba ya Watumishi ameishukuru Serikali kwakuona TDB kuwa inastahili kupata Tuzo hii kwani inaonesha kuwa Taasisi inatimiza jukumu lake la Msingi katika kuwahudumia Wadau wa Tasnia ya Maziwa nchini.
Maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yaliyokuwa yanafanyika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma kuanzia Agosti Mosi, 2025 yalihitimishwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo Bodi ya Maziwa Tanzania iliibuka Mshindi wa kwanza katika kundi la Bodi za Mazao ya Mifugo