TDB YATOA ELIMU YA BIASHARA, USAJILI, NA UWEKEZAJI KWENYE TASNIA YA MAZIWA
Bodi ya Maziwa Tanzania Aprili 24, 2023 imetoa elimu ya Biashara, usajili na uwekezaji kwenye tasnia ya maziwa kwa washiriki wa mafunzo ya usindikaji wa vyakula mbalimbali ikiwemo maziwa kwa washiriki wapatao 380 jijini Dodoma chini ya Shirika la Wanawake na Uchumi wa Viwanda (WAUVI) Mkoa wa Dodoma yaliyoratibiwa na Shirika la kuwahudumia viwanda vidogovidogo (SIDO).
Katika mafunzo hayo yaliyodumu Kwa siku 4 Kaimu Meneja Masoko toka Bodi ya Maziwa Tanzania Bw. Joseph Semu alipata wasaa wa kuwapitisha washiriki hao kuwaonesha fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye tasnia ya maziwa ambapo amewaeleza kuwa Tanzania bado kuna uhitaji mkubwa wa soko la maziwa kwani Tanzania inatumia fedha nyingi kuagiza maziwa toka nje.
Bwana Semu amewahamasisha washiriki wa mafunzo hayo kujikita katika tasnia ya maziwa baada ya kupata elimu ya usindikaji maziwa kwani soko lake ni kubwa hapa nchini itawasadia kujikwamua kiuchumi na kuongeza pato la Taifa letu kwani inashauriwa kutumia lita zipatazo 200 kwa mtu mmoja katika kipindi cha mwaka mzima.
Vilevile ametumia fursa hiyo kwa niaba ya Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwakutoa kiasi cha Tsh. Bilioni 2 Kwa ajili ya kujenga vituo vya kukusanyia maziwa nchi nzima ambavyo vitawarahishia wafugaji wetu kuwa na sehemu za kupeleka maziwa yao hivyo kuwa na uhakika wa soko la maziwa.
Mafunzo hayo yakiwa ni ya awamu ya tatu kufanyika yaliyotanguliwa na kundi la kutengeneza sabuni na batiki yalifungwa rasmi na Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Dodoma Mh. Fatma Taufiq.