UNYWAJI MAZIWA KWA WANAFUNZI SHULENI NI MATOKEO YA AFYA BORA -RAS GEITA

Katibu Tawala Mkoa wa Geita Ndg. Mohammed Gombati amesema kuwa unywaji wa maziwa safi na salama kwa wanafunzi shuleni kutaongeza ufaulu na Afya Bora kwa wanafunzi Mkoani Geita.
Ndg.Mohammed Gombati ameyasema hayo wakati akifungua Kongamano la wadau wa Tasnia ya Maziwa Septemba 23, 2025 katika Ukumbi wa Nyerere Uliopo katika Viwanja vya Maonesho vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Uliopo Manispaa ya Geita.
Ndg.Mohammed Gombati amesema viongozi, walimu, wazazi na walezi ni wadau muhimu wa kuhakikisha watoto wanakunywa maziwa wakiwa shuleni na kuhakikisha zoezi hili linakuwaendelevu ili wanafunzi waondokane na tatizo la udumavu wa mwili na akili.
Katibu Tawala Mkoa wa Geita amewasisitiza maafisa lishe kuelimisha jamii kuhusu lishe Bora na matumizi ya maziwa safi na salama.
Aidha amewaagiza maafisa mifugo kuwahamasisha wafugaji, kufuga kisasa Ili wawezeshe upatikanaji wa maziwa kwa muda wote.
Ndg. Gombati ametoa wito kwa washiriki wa kongamano kutoa maoni ya kujenga mpango mzuri wenye kuleta tija kwa Taifa.
Naye Kaimu Msajil wa Bodi ya Maziwa Tanzania Bi. Deorinidei Mng'ong'o, amesema Kongamano hili litajadili mpango mahususi na endelevu wa kuhakikisha watoto shuleni wanakunywa maziwa Ili kukuza ustawi wa afya ya mwili na akili.
Kongamono hilo limeongozwa na Kauli kauli mbiu isemayo "Kwa matokeo Mazuri Shuleni na Afya Bora, Maziwa Ndio Mpango Mzima"