Taratibu za uingizaji wa maziwa na bidhaa za maziwa nchini
Utaratibu wa kutoa/kuingiza maziwa ndani au nje ya nchi
Bodi ya Maziwa ya Tanzania hutoa vibali vya kuagiza na kuuza nje maziwa na bidhaa za maziwa kama ilivyoelezwa katika Kanuni ya Maziwa (Uingizaji na Uuzaji wa Maziwa na Bidhaa za Maziwa) ya mwaka 2011. Lengo ni kufuatilia mwenendo wa uzalishaji wa maziwa ndani ya nchi, uuzaji wa maziwa na mahitaji ya kuagiza maziwa.
Mahitaji ya Msingi
- Leseni ya biashara
- Cheti cha usajili wa bidhaa kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
- Cheti cha usajili wa jengo kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
- Namba ya mlipa kodi
Maombi ya kutoa na kuingiza maziwa ndani au nje ya nchi
Mtu yeyote kabla ya kuagiza / kuingiza maziwa na bidhaa za maziwa anapaswa kuomba kibali kutoka kwa Msajili wa Bodi. Utaratibu wa kupata kibali unahitaji mwombaji kujaza na kuwasilisha fomu ya maombi ya kuingiza na kutoa maziwa ndani au nje ya nchi kwa Msajili ikiwa na nyaraka zifuatazo;
- Ankara ya malipo
- Cheti kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo
- Orodha ya bidhaa zilizopakiwa
Fomu ya maombi ya kuingiza na kuagiza inapatikana katika ofisi za Bodi za Maziwa na inaweza kupakuliwa kutoka kwenye tovuti.
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na Bodi ya Maziwa Tanzania kupitia anwani zilizopo kweny tovuti.