TUKUTANE MWANZA MEI 28 - JUNI 01
Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe toka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt Nyamizi Bundala akitoa neno la utangulizi kuhusu Mkutano wa Usambazaji wa Nakala za Mpangokazi wa Utekelezaji wa Programu ya Unywaji Maziwa Shuleni pamoja na makabidhiano ya vibanda vya maziwa vitakavyotumika kutoa huduma ya maziwa shuleni wakati wa Mkutano huo uliofanyika Machi 27, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa OSHA mkoani Dodoma.
Mkuu wa Masuala ya Lishe UNICEF Bw. Patrick Codjia akitoa salamu za UNICEF na kuelezea namna Shirika hilo lilivyoshirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika hatua zote za maandalizi ya Mpangokazi wa Programu ya Unywaji Maziwa Shuleni na Utengenezaji wa Vibanda vitakavyotoa huduma ya Maziwa Shuleni aidha alibainisha usambazaji wa Mpangokazi huo ni hatua muhimu ya utekelezaji wa Mpangokazi Jumuishi wa Lishe Kitaifa ambapo Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeweka viashiria vyakuhakikisha mazao ya mifugo na uvuvi yanatumika kuboresha hali ya lishe nchini katika Mkutano wa Usambazaji wa Nakala za Mpangokazi wa utekelezaji wa programu ya Unywaji Maziwa Shuleni uliofanyika Machi 27, 2024 katika Ukumbi wa mikutano wa OSHA.
Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Prof. George Msalya akitoa maelezo ya jumla kuhusu mchakato wa uandaaji wa Mpangokazi wa Utekelezaji wa programu ya Unywaji Maziwa Shuleni pamoja na yaliyomo ndani ya Mpangokazi huo na namna ambavyo Mpangokazi huo umezingatia ushiriki na ushirikishwaji wa Wadau, Uratibu na Uendelezaji wa Mpango huo katika Mkutano wa Usambazaji wa Nakala wa Mpangokazi huo uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa OSHA mkoani Dodoma Machi 27, 2024.
Naibu Katibu Mkuu Mifugo Prof. Daniel Mushi akielezea namna Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilivyofanikisha kuinua kiwango cha uzalishaji maziwa nchini na namna ilivyojipanga kuhakikisha maziwa hayo yanatumika kuimarisha usalama wa chakula, kuboresha hali ya lishe, kuinua kipato cha wafugaji na wadau katika mnyororo wa thamani wa maziwa sambamba na kukuza soko la ndani la maziwa, wakati akifungua Mkutano wa Usambazaji wa Nakala za Mpangokazi wa Utekelezaji wa Programu ya Unywaji Maziwa Shuleni pamoja na makabidhiano ya Vibanda vitakavyotoa huduma ya maziwa shuleni uliofanyika Machi 27, 2024 katika Ukumbi wa OSHA mkoani Dodoma.
SIKU YA WANAWAKE DUNIANI "WEKEZA KWA WANAWAKE HARAKISHA MAENDELEO YA TAIFA NA USTAWI WA JAMII"
Pichani ni sehemu ya washiriki wa hafla ya kukabidhi Ng’ombe kwa Kampuni ya Kahama Fresh iliyofanyika katika shamba la Mifugo la Kampuni hiyo lililopo wilayani Karagwe, mkoani Kagera Januari 23, 2024.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na kikundi cha kina mama wanufaika wa programu ya Kopa Ngombe Lipa Maziwa muda mfupi baada ya kuzindua programu hiyo iliyofanyika kwenye shamba la Mifugo la Kampuni ya Kahama Fresh lililopo wilayani Karagwe, mkoani Kagera Januari 23, 2024.
Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Prof. Goerge Msallya akitoa neno fupi kuhusu Tasnia ya Maziwa katika hafla ya kukabidhi Ng’ombe kwa Kampuni ya Kahama Fresh iliyofanyika katika shamba la Mifugo la Kampuni ya Kahama Fresh lililopo wilayani Karagwe, mkoani Kagera Januari 23, 2024.