Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Nyama na Bodi ya Maziwa (hawapo pichani) wakati wa kikao kilichofanyika jijini Dodoma Mei 7, 2024, ambapo alipokea taarifa za utekelezaji wa bodi hizo ambazo kwa sasa zimeunganishwa na kuundwa taasisi moja itakayosimamia mazao hayo ya mifugo.
Msajili wa Bodi ya Maziwa Prof. George Msalya akitoa neno la Utangulizi mbele ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Ulega (hayupo pichwani) wakati wa kikao kilichofanyika jijini Dodoma Mei 7, 2024 kilichojumuisha Bodi ya Maziwa na Bodi ya Nyama, ambapo kwenye kikao hicho Mhe. Waziri alipokea taarifa za utakelezaji wa bodi hizo ambazo kwa sasa zimeunganishwa na kuundwa Taasisi moja itakayosimamia Mazao ya hayo ya Mifugo
Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha
TUKUTANE MWANZA MEI 28 - JUNI 01
Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe toka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt Nyamizi Bundala akitoa neno la utangulizi kuhusu Mkutano wa Usambazaji wa Nakala za Mpangokazi wa Utekelezaji wa Programu ya Unywaji Maziwa Shuleni pamoja na makabidhiano ya vibanda vya maziwa vitakavyotumika kutoa huduma ya maziwa shuleni wakati wa Mkutano huo uliofanyika Machi 27, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa OSHA mkoani Dodoma.
Mkuu wa Masuala ya Lishe UNICEF Bw. Patrick Codjia akitoa salamu za UNICEF na kuelezea namna Shirika hilo lilivyoshirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika hatua zote za maandalizi ya Mpangokazi wa Programu ya Unywaji Maziwa Shuleni na Utengenezaji wa Vibanda vitakavyotoa huduma ya Maziwa Shuleni aidha alibainisha usambazaji wa Mpangokazi huo ni hatua muhimu ya utekelezaji wa Mpangokazi Jumuishi wa Lishe Kitaifa ambapo Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeweka viashiria vyakuhakikisha mazao ya mifugo na uvuvi yanatumika kuboresha hali ya lishe nchini katika Mkutano wa Usambazaji wa Nakala za Mpangokazi wa utekelezaji wa programu ya Unywaji Maziwa Shuleni uliofanyika Machi 27, 2024 katika Ukumbi wa mikutano wa OSHA.
Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Prof. George Msalya akitoa maelezo ya jumla kuhusu mchakato wa uandaaji wa Mpangokazi wa Utekelezaji wa programu ya Unywaji Maziwa Shuleni pamoja na yaliyomo ndani ya Mpangokazi huo na namna ambavyo Mpangokazi huo umezingatia ushiriki na ushirikishwaji wa Wadau, Uratibu na Uendelezaji wa Mpango huo katika Mkutano wa Usambazaji wa Nakala wa Mpangokazi huo uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa OSHA mkoani Dodoma Machi 27, 2024.
Naibu Katibu Mkuu Mifugo Prof. Daniel Mushi akielezea namna Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilivyofanikisha kuinua kiwango cha uzalishaji maziwa nchini na namna ilivyojipanga kuhakikisha maziwa hayo yanatumika kuimarisha usalama wa chakula, kuboresha hali ya lishe, kuinua kipato cha wafugaji na wadau katika mnyororo wa thamani wa maziwa sambamba na kukuza soko la ndani la maziwa, wakati akifungua Mkutano wa Usambazaji wa Nakala za Mpangokazi wa Utekelezaji wa Programu ya Unywaji Maziwa Shuleni pamoja na makabidhiano ya Vibanda vitakavyotoa huduma ya maziwa shuleni uliofanyika Machi 27, 2024 katika Ukumbi wa OSHA mkoani Dodoma.
Pichani ni sehemu ya washiriki wa hafla ya kukabidhi Ng’ombe kwa Kampuni ya Kahama Fresh iliyofanyika katika shamba la Mifugo la Kampuni hiyo lililopo wilayani Karagwe, mkoani Kagera Januari 23, 2024.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na kikundi cha kina mama wanufaika wa programu ya Kopa Ngombe Lipa Maziwa muda mfupi baada ya kuzindua programu hiyo iliyofanyika kwenye shamba la Mifugo la Kampuni ya Kahama Fresh lililopo wilayani Karagwe, mkoani Kagera Januari 23, 2024.